Friday, September 20, 2024

NGUVU YA MAOMBI

Maombi ni mawasiliano baina ya pande mbili.
“Maombi kwa MUNGU” yaani kumwomba Mungu ni mawasiliano baina ya mwanadamu na Mungu ambayo huimarika katika majawabu yatokayo kwa Mungu.

Lengo la somo hili ni kuhimarisha mawasiliano yako na Mungu katika maombi.

Katika somo hili tutaenda na Yakobo 1:5-7

Yakobo 1:5-7; “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.”

Pia maombi ni mhimu sana yaambatane na imani maombi yoyote yale yasipokuwa na imani ni sawa na bure. Maombi ya imani ni yale yasiyo kuwa na shaka ndani yake. Sio shaka tu bali shaka ya aina yoyote maana ukiomba kwa shaka kamwe hauta pokea kwa Bwana.

Waebrania 11:1; “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”

Na kumbuka kwamba maana ya uhakika ni kutokuwa na mashaka au wasiwasi wa aina yeyote ile. Na uhakika unakuthibitishia ya kwamba kile unacho kiomba au kitarajia ni lazaima kipo au kinakuja.

Ukiwa na mashaka katika maombi tambua moja kwa moja ya kuwa hauna imaani. Na kama hauna imani usitegemee kupokea majibu kutoka kwa Bwana maana Bwana huwajibu wale wanao mwamini katika maombia yao.

Ndiyo ni kanuni yake mwenyewe Mungu wetu.

Mungu anafanya kazi yake kwa kanuni na kama unataka kuishi maisha anayotaka lazima ukubaliane nazo.

Uombapo usiombe kwa mashaka maana mashaka ni kama wimbi

Na sifa ya Wimbi ni kufuata mwelekeo a upepo unako elekea hivyo kama upepo ukivuma kutoka kaskazini kwenda mashariki wimbi hufuata na kama upepo ukigeuza kutoka kaskazini kwenda kusini wimbi nalo hufuata ndivyo alivyo mtu wa mashaka.

Kwahiyo mtu wa tabia kama hizi katika maombi asidhani ya kuwa atapokea kwa Bwana.

…oooh Bwana Yesu asifiweee…

Maombi yenye imani pasipo mashaka ni kama kutembea huku ukienda sehemu unayo ifahamu

kwa mfano mtu anaye tembea kwenda kwao anapo pafahamu uwe na uhakika hawezi kupotea hata siku moja hii ni kwa sabau anafahamu anapo kwenda.

Ndivyo yalivyo na mambi yasio na shaka kwa kuwa humfanya mtu atembee huku akitegemea kupokea kile alicho kiomba kwa Bwana.

Unatakiwa uombe kwa imani pasipo mashaka maana mashaka mashaka yatakufanya usipokee.
Mimi sijui ni wakristo wa ngapi ambao huandika maombi yao huku waki yawekea vema kwa yale yanayo jibiwa ila ninacho kifahamu ni kwamba wengi huwa wanaomba juujuu tu huku wakizani ya kuwa Mungu amesha wajibu kumbe bado wanaishia pasipo kuona matokeo ya kile wanacho kiombea na hii nikutokana na kutokuamini kwao.

Nasema kwa sababu ya kutokuwa na imani kwa sababu kama wangeomba kwa imani nilazima wangepokea kutoka kwa Bwana.

Kumbuka si kuomba tu kwa ajili ya mapepo na wachawi bali Biblia katika Yakobo inatueleza ya kuwa hata ukipungukiwa na hekima napo unatkiwa kwenda kwa Mungu ili akupatie hekima ipitayo hekima zote za kibinadamu, ili uipokee hekima hiyo au lolote uliombalo unacho takiwa kufanya ni kuomba kwa imani timilifu..

Wagalatia 3:7; “Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.”

Neno linathibitisha yakuwa wale walio na imani hao ndio wana wa Ibrahimu. Kumbuka katika agano jipya tunazipata ahadi za Mungu alizo mwahidi Ibrahimu kupitia Yesu kristo kwa njia ya imani.

Unapo isoma Biblia unatambua ukweli kabisa ya kwamba Ibrahimu aliitwa baba wa imani na kuwa rafiki wa Mungu kwa sababu ya kuamini hivyo hata wewekama unahitaji kuwa rafiki wa karibu wa Mungu ni lazima utembee kwa kumwamini yeye kwa kila ulitendalo.

Kumbuka sio kuamini kwa wasiwasi bali kuamini kwa Imani timiifu isiyo na mashaka ndani yake.

Katika maombi ipo siri ya ajabu sana ambayo imefichika katika Imani kwa kile unacho taka Mungu akujibu jitahidi sana kuomba kwa imani maana pasipo imani kamwe haiwezekani kumpendeza Mungu siri hii itakusaidia sana kama utaiweka katika uhalisia wa vitendo.

Katika maisha ya wokovu nimeona majibu ya maombi yangu yakijibiwa kwa haraka sana pale nilipokuwa nikiomba kwa imani, hivyo mpendwa kama unataka kujibiwa maombi yako usihangaike kutafufuta jawabu lingine tofuti na kuomba kwa imani; maana katika imani ndimo kuna majibu tosha ya maombi yako.

Kitu kingine ninacho kushirikilisha ni kuhusu

Kuishi kikamilifu katika maisha ya wokovu maana kuna nguvu ya kipekee sana inayo chochea maombi ya imani nayo inatoka katika Roho Mtakatifu ambaye huwa ndani ya wale wote wanaoishi maisha ya kumtegemea Mungu pasipo kufuata tamaa za mwili.

Hivyo unapo ishi maisha matakatifu Roho Mtakatifu atakusukuma kuomba kwa mzingo na kwa imani katika maombi yako yote haswa yaliyo mapenzi ya Mungu kwako.

FUNGUO TATU ZA YESU ALIZOTUPA KUHUSU MAOMBI YENYE MAJIBU:
Pia kuna funguo tatu au mambo matatu ambayo Yesu ameyatoa ili kupata majibu yetu katika maombi nitaelezea moja baada ya nyingine.

1. USTAHIMILIVU (USUGU):
Funguo ya kwanza ya kujibiwa maombi ni ustahimilivu (kung’ang’ania).

Mungu anatutaka sisi kushikilia ipasavyo ahadi zake katika maombi. Maombi yetu yote yajengwe kwenye ahadi zake yeye.

Luka 11:10; “Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.”

Sasa maana yake nini?

Omba na uendelee kuomba utapewa. Tafuta na uendelee kutafuta utapata. Bisha na uendelee kubisha mlango na utafunguliwa.

Tukimuomba Mungu ameahidi kutupa Lakini inabidi tusubirie wakati sahihi wa Mungu. Maandiko yanasema yeye hawahi wala hachelewi…

2. MAKUSUDI (BE PURPOSEFUL):
Biblia inasema sababu kubwa ya sisi kutokupokea vipawa vya Mungu ni kwa sababu hatujaomba.

Yakobo 4:2; “Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!”

Zaburi 37:4-5; “Nawe utajifurahisha kwa BWANA, Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.”

3. MAHUSIANO NA BABA (PERSONAL RELATIONSHIP):
Kitu cha muhimu sana kwenye maombi yenye majibu ni mahusiano mazuri na baba wa mbinguni.

Watu wawili kwenye biblia ambao wanasifiwa au wanaonekana kuwa na Imani kubwa ni Musa na Ibrahimu.

Lakini wawili hawa walifanikisha njia yako kwa sababu walikuwa na mahusiano ya kipekee na Mungu.

Yakobo 2:23; “Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.”

Kutoka 33:11; “Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.”

Watu hawa walifanya maajabu ulimwenguni.

KWANINI WALIFANYA MAAJABU?

Lakini kumbuka inachukua muda kuwa na mahusiano ya karibu sana na Mungu.

Unaanza kwa kumhusisha Mungu kwenye mambo ya maisha yako ya kila siku.

Tenga muda maalumu kwa ajiri ya usomaji wa biblia.

Anza kuombea rafiki zako pia kumbuka kumshukuru Mungu kwa yale ambayo anajibu kila siku.

Naomba nifikie kikomo hapa kwa leo, Mungu akitujaalia wakati mwingine tutasemezana.

Bwana Mungu awabariki sana!
Inakuja: Vipawa na karama za roho Mtakatifu, kaa tayari kwa ajili ya mafundisho itakayo kuja. 
MS. GUILLAIN 

SIFA NA MAABUDU (New Generation)

Sifa na kuabudu ni maneno yenye maana inayokaribiana. Kusifu ni kueleza wasifu wa mtu au kitu. Kwa maana nyingine ni Kumuinua Mungu juu, ni Kushukuru na Kumpazia sauti, kumfanyia shangwe na kujishusha chini ya Bwana Yesu kwa Unyenyekevu. Kuabudu maana yake Kusujudia, kuinama kwa kuonesha unyenyekevu, heshima kwa au kuanguka kifudifudi. Kusifu na kuabudu ni agizo la Bwana kwa wanadamu. Ni katika sifa Mungu uwatokea wanadamu. Mungu akishuka katikati ya wanadamu siku zote huleta mabadiliko.

 Zamani makanisa ya kiroho yalijulikana kwa kumsifu Mungu na hata sasa. Kumsifu na kumwabudu kwa moyo wa kweli kunavuta mtu kwa Mungu. Siku zote Mungu anapenda kusikia, tukiisifia kazi na uumbaji wake na mambo makubwa aliyotenda maishani mwetu. Ni kawaida hata wanadamu wanapenda kusifiwa. Mfano kila mwajiri anapenda kusifiwa na wafanyakazi wake jinsi anavyowatendea au jinsi alivyo bos mzuri. Mungu ni zaidi ya wanadamu wote maana yeye ndiye aliyewaumba wote na sisi tu watu wake.

KUSIFU NI AGIZO LA MUNGU
Zaburi 34:1 Imeandikwa, “Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima. 2 Katika Bwana nafsi yangu itajisifu, Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.3 Mtukuzeni Bwana pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja.” Kuabudu na kumsifu Mungu ni jambo la siku zote na nyakati zote. Unaweza kumsifu na kumwadhimisha Mungu ukiwa safarini, kazini, shambani au mahali popote. Kumsifu Mungu kunasababisha mtu ahisi uwepo wa Mungu. Kusifu na kumwabudu ni mahali pote bila kujali hali uliyo nayo. Kuna wakati mwingine ambao unapita wakati mgumu hata huwezi kuomba. Lakini jipe moyo na umwimbie Mungu. Anza kumsifu Mungu kwa kuimba kwa sauti yako, kwa kupiga kinanda, zeze na zumari. Mwingine anaweza kupiga vigelele na miluzi pia. Katika kumsifu Mungu hakuna kuangalia nafasi uliyonayo katika jamii.

Yohana 4: 4-24 Imeandikwa, “ Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria. 5 Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe. 6 Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita. 7 Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. 8 Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. 9 Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.)10 Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. 11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? 12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? 13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; 14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka. 16 Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. 17 Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; 18 kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. 19 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! 20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. 21 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

Hizi ni habari za mwanamke aliyekuwa anatafutwa na Yesu. Huyu ni mama aliyekuwa na matatizo ya kuolewa na kuachwa. Ila Yesu akamuuliza maswali mpaka akamfahamu asili yake. Mtafute Yesu na utamfahamu kwa undani zaidi. Kumwabudu Mungu ni sawa na kuomba, katika kumwabudu Mungu roho ya mwanadamu inakutana na Roho wa Mungu. Imeandikwa Mungu ni roho, na wale wamwabuduo lazima wamwabudu katika roho na kweli.

Mathayo 15 : 8- 9 Imeandikwa, “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. 9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.” Kumbe ili umwabudu Bwana lazima uwe na Bwana Yesu ndani yako. Moyo uko tayari kuyatenda mapenzi ya Mungu. ndio maana neno linasema ipo saa ambayo wamwabuduo Mungu watamwabudu katika roho na kweli. Kumwabudu Mungu katika kweli ni kuishi katika Haki. Neno la Mungu linasema watu hawa wananiheshimu kwa midomo ila mioyo yao iko mbali nami. Unaona Yesu anamtafuta mtu mmoja amabaye moyo wake ameuweka tayari kwa ajili ya Bwana Yesu.

2 Nyakati 5: 13-14 Imeandikwa, “hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana,14 hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.”

Mungu anamtafuta mtu atakayemwabudu katika Roho na Kweli. Kusifu na Kumwabudu Mungu kunafanyika katika Roho na kweli. Anachoangalia Mungu ni kile kinacho kusukuma kumchezea Bwana Yesu. akitupata wote, tukimwabudu tunakuwa tumeungana na Roho wa Mungu. Tukishaunganika kwa pamoja tukiimba, na tukiomba Nguvu ya Mungu itaonekana kwa namna ya tofauti. Zaburi 22: 3 Imeandikwa,” Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.” Tukiungana kwa pamoja basi Mungu hutokea na kuketi katikati yetu. Mathayo 18: 20 Imeandikwa, “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” Tukimwabudu kwa pamoja Mungu ushuka kwa nguvu na uweza wake wote. Na Mungu akishuka tayari uponyaji unadhihirika. Mtu yeyote katika maisha anatamani uwepo wa Mungu. Maana uwepo wa Mungu ukiwepo, mtu uwa na amani kwa kila analolifanya. Kwa sababu uwepo wa Mungu ukiwepo, kazi, biashara, masomo, huduma inakuwa salama.

SIFA HUFUNGUA VIFUNGO;

Matendo ya Mitume 16:23-28 Imeandikwa, “Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. 24 Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. 25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. 27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. 28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.”

Katika sifa miujiza hutokea, ni katika sifa tu hata yale yasiyowezekana kwa macho ya wanadamu, yanawezekana. Hapa Paulo na Sila walikuwa gerezani. Ni wafungwa waliompiga mkuu wa mji aliyewapatia mabwana zake mali kwa nguvu za kishetani. Hawa ni wafungwa waliokuwa wafungwa maaalumu. Kwa kawaida kila mlango wa gereza huwa na kufuli. Wakaingizwa chumba maalum, wakafungwa kwa mikatale ili wasitoroke. Wakawekewa walinzi. Lakini cha kushangaza watumishi hawa waliijua siri ya kusifu na kuabudu. Hawakuangalia hali ya tatizo walilokuwa nalo. Bali katika hali ya vita ile walianza kumsifu Mungu
Neno la Mungu linasema walimsifu Mungu kwa furaha. Kuna mambo ambayo umeyaombea mpaka umechoka sana. Usikate tama, bali ndio wakati wa kuanza kuimba na kumsifu Bwana.  Kwenye kuimba lazima utakutana na Mungu. Kupitia sifa Mungu atakutana na hitaji la moyo wako nawe utakuwa salama kwa jina la Yesu. Wafungwa wengine waliwashangaa sana kwa maombi yale. Kumbe kuna tatizo ambalo halijaisha kwa sababu hujamwabudu Mungu. Mungu aliiangalia Imani yao. Baada ya muda mfupi misingi ya gereza ilitikisika na milango ya gereza ikafunguka. Kushinda kwao kulitokana na kumsifu na kumwabudu Bwana.

Yona 2: 1-7 Imeandikwa, “Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, 2 Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu,  Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba,  Nawe ukasikia sauti yangu. 3 Maana ulinitupa vilindini,  Ndani ya moyo wa bahari;  Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu. 4 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;  Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu. 5 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;  Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu; 6 Nalishuka hata pande za chini za milima;  Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele;  Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni,  Ee Bwana, Mungu wangu, 7 Roho yangu ilipozimia ndani yangu,  Nalimkumbuka Bwana;  Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu.

Yona aliwai kuwa ndani ya tumbo la Samaki. Katika tumbo Yona hakuwa na maamuzi juu ya maisha yake, hili lilikuwa gereza. Hiki kilikuwa kifungo cha aina yake. Yona alipokuwa katika tumbo la Samaki, akamlilia Bwana. Yona alimsifu na kumwabudu Bwana ndipo alipotapikwa kutoka tumboni mwa Samaki. Siri ya kufunguliwa kwa Yona, ilikuwa ni kumsifu Bwana. Baada ya kumsifu na kuabudu ndipo Bwana akamwamuru samaki amtapike Yona. Katika shida yako uelekeze moyo wako kwa Bwana. Mtafute Bwana nyakati zote. Usiifanye shida yako kuwa ndio sehemu ya maamuzi yako. Mwabudu na kumsifu Mungu ili ashuke kukusaidia. Yona alipokuwa katika vilindi vya bahari akakumbuka kwa habari za waliowai kusaidiwa na Mungu. Lazima tujifunze kumwabudu Mungu katika hali zote. Kuliangalia tatizo na kukata tamaa ni kumtukuza shetani. Hii ni kwa sababu mabaya utoka kwa shetani. Yakiwepo magumu mbele yako, mwabudu Mungu nawe katikati ya sifa utapata ufumbuzi wa tatizo lako.

Zaburi 149: 1-6 Imeandikwa, “Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa. 2 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao. 3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa
matari na kinubi wamwimbie. 4 Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu. 5 Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao. 6 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao
.” Tukiabudu Mungu hushuka. Uwepo wa Mungu ukiwepo mahali kila kitu utikiswa. Ndio maana Yesu alipofufuka makaburi yote yalipasuka na wafu wakatoka.  Jifunze na tufanye kumsifu na kumwabudu Mungu kuwe sehemu ya maisha yetu. Kumsifu Mungu kunasababisha miujiza na nguvu ya Mungu kuonekana katika maisha yako.
Imeandikwa na Mudadi Saidi
Barikiwa