Wednesday, April 20, 2022

Maana ya ndoto kiroho,sehemu ya pili

Ujambo mpendwa katika Kristo Yesu, ninakuja tena kwa mara nyingine kukuleteya somo hii “MAANA YA NDOTO KIROHO” THE MEANING OF DREAM SPIRITUALLY, party 2

www.mountmoriahministry.blogspot.com

Na, MS. Guillain 

Karibu tena kwa somo, Katika sehemu hii ya pili tunakwenda kuangalia mambo makuu mawili, ambayo ni;
Aina za NDOTO ni zipi?
Namna ya kutambua NDOTO tunazoota ni ipi?

Aina Za Ndoto na tofauti zake:

Ni muhimu sana kujifunza aina za ndoto kwasababu, hizo aina ndizo zitatuongoza namna ya kuzikabili. Zipo aina kuu MBILI za NDOTO;
Ndoto za KIMWILI
Ndoto za KIROHO

A) Ndoto Za Kimwili:

“Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.” Mhubiri 5:3

Hizi ndoto huitwa PUMZIKO LA MWILI. Baada ya mwili kufanya kazi sana haswa kwa kutumia ile milango mitano ya fahamu; macho, pua, ulimi, ngozi na masikio.

Usiku unapolala; ni MWILI ndiyo unaolala bali MOYO (Roho na Nafsi) zinakuwa zinaishi. Picha ya mambo uliyoyafanya kwa matendo au kwa kuyafikiria inajirudia katika NJOZI, nayo inakuwa inaitwa ndoto za kimwili. Kwa wale wanaongaliaga movie za kutisha utakuta usiku ukiwa umelala unaota ndoto nawe umo katika wakati wa vitisho kama ulivyoangalia kwenye movie

Au unakuta ulikuwa unafikiria jambo, unatumia nguvu nyingi katika kufikiria. Unajikuta usiku unaota ndoto inayotokana na mawazo yako. Lakini pia hizi ndoto zinaweza kukutokea kwasababu za kiafya au ukuaji wa mwili. Ukia mgonjwa mwili unakuwa na uchovu sana hivyo unapata usingizi mzito kama pumziko nako unakupelekea kupata ndoto. Katika hatua fulani za ukuaji mwanadamu anakuwa anaota ndoto mbalimbali kama kuokota fedha, kurukia bondeni, kutembea kenye kivuko kidogo sana majini nk.

Sifa yake kubwa ni kwamba unapoota hiyo ndoto; inakuwa haikusonineshi wala haina mguso wa ndani wowote… Tofauti na ndoto za KIROHO.

B) Ndoto Za Kiroho:

Ayubu 33:14-16 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,”

Ndoto za kiroho unapoziota, zinakuja kwa mguso wa ndani ya moyo wako. Unakuta ni ndoto ya kawaida sana ila unapoiota inaanza kukupa msononeko sana. Unakuta unaota ndoto alafu baada ya ndoto ikaanza kukutesa sana moyo mwako. Hiyo ndoto usiipuuze; bali ipokee na kuihoji

Tabia ya muhimu nyingine ya ndoto za kiroho ni kwamba zinakuwa na msisitizo ndani yake… Utaiota mara ya kwanza, na mara ya pili na hata zaidi ya hapo.

Lakini zipo aina MBILI za NDOTO hizi za KIROHO; Nazo ni muhimu sana kuzitofautisha.

Aina MBILI za NDOTO ZA KIROHO ni:-
Ndoto za MUNGU
Ndoto za SHETANI

Mwanzo 40:5-7 “Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika. Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?”

Hawa jamaa wawili, Yusufu aliwakuta wakiwa WAMEFADHAIKA asubuhi…. Kisa tu ni kuota NDOTO.

Mwanzo 28:16-19 “Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.”

Yakobo akaogopa na akaondoka asubuhi na mapema sana.

Mwanzo 41:8 “Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.”

Roho ya Farao ilifadhaika sana baada ya kuota ndoto. Farao pia aliota ndoto hata mara mbili na ndivyo ndoto za kiroho zilivyo, zinakuwa na mkazo ama za msisitizo. Biblia inasema, “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;” Ayubu 33:14-15.

Ndoto za Mungu zinaitwa mara pengine kama ndoto za ufalme mkuu wa mbinguni (ufalme wa nuru) na ndoto za shetani zinaitwa tena ndoto za ufalme wa kuzimu (ufalme wa giza)

SWALI LINAKUJA: Unawezaje kutofautisha NDOTO YA MUNGU na NDOTO YA SHETANI?

Ndoto za kuroho ni malango ya kiroho ya Mungu kusema nawe au shetani kusema nawe. Zina madhara makubwa sana kimwili na kiroho.

Ili uweze kuzifanyia kazi NDOTO, unapaswa KUZICHUNGUZA kwa umakini sana. Siyo ndoto zote zinamaana kiroho, zingine ni ndoto za kimwili tu ambazo hazina maana sana za kufanyiwa kazi.

Sasa, Je utazitofautishaje??? Na kuzitofautisha ni lazima ili kuweze kuzikabili ndoto.

Ndoto za kimwili unapaswa kuzipuuza na kuzitupilia mbali; ila ndoto za kiroho zinahitaji kufanyiwa kazi mara moja. Sasa; Nitazitofautishaje hizo ndoto?

NDOTO ZA KIROHO tumesema ni MALANGO (OPENING) ya KIROHO ambayo ulimwengu wa kiroho unatumia kuwasiliana nawe. Shetani anaweza kutumia ndoto kupandikiza vitu kwako ambavyo usipovingoa vinaweza kwamisha maisha yako.

“Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema, Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong’ono yake. Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu. Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote. Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama. Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena. Ayubu 4:1, 12-16.

Hapa kuna vitu vinne; yaani kuna:-
WAZO liliingia ndani yake kwa NDOTO.
Katika MASIKIO iliingia SAUTI iliyoharibu usikivu wake.
HOFU ilimwingia.
Mifupa yake ikaanza kutetemeka.

Kumbuka IMANI ni kuwa na HAKIKA na mambo yatarajiwayo. Ni bayana ya mambo yasiyoonekana. IMANI chanzo chake ni KUSIKIA; na kusikia huja kwa NENO la Kristo.

Kupitia NDOTO ZA KIROHO Mungu anakuwa anasema nawe:-
Ili kukupa taarifa Fulani
Ili kukuonya kwa jambo Fulani
Ili kukupa tahadhari fulani

Pia ni kupitia NDOTO ZA KIROHO shetani anakuwa anasema nawe:-
Ili kukudhoofisha
Ili kukutesa
Ili kukutoa katika uwepo wa Mungu

Usiipuuzie ndoto unayoota maana inaweza tumika; kukuletea ujumbe wa Mungu, Maonyo au shetani anaweza pandikiza vitu. Mara nyingi shetani hatakuja na NDOTO tu, atakuja na ISHARA na utampokea kwa sababu ya ISHARA au MUUJIZA.

Na yeye ataleta na ujumbe na itakuwa ngumu sana kwako kukataa kwa sababu umeona ISHARA au MUUJIZA. Na lengo kubwa ni kuwa “uache kumfuata Mungu” na “kumpenda Mungu kutapoa” na “utapoteza hofu ya Mungu”

Shetani akifanikiwa katika hiyo dhamira yake kupitia NDOTO; Unapoteza kuambatana na Mungu. Unatopeteza kusikia Mungu anachosema na utaanza kupotea na utaanza kusikia neno la mtumishi zaidi bila kufuata neno la Mungu. Na wengi wamekwama hapo. Wapo watumishi wameacha kumtumikia Mungu kwa sababu waliota NDOTO na kuna vitu vilikuja na mbwembwe na wakidhani ni Mungu kumbe wala siyo MUNGU.

“Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye. Kumbukumbu la Torati 13:1-4

Ndoto inaweza tumika na shetani:-
Kupandikiza unabii wa uongo kwa kutumia ishara.
Wanapewa uwezo wa kushawishi watu wasimfuate Mungu katika Kristo Yesu.

NDOTO ZA MUNGU unaweza sana kuzitofautisha na NDOTO ZA SHETANI. Kama unaota ndoto inakupa VITISHO katika maisha yako ya kiroho ama kimwili; ujue kabisa umetoa nafasi kwa SHETANI kusema nawe.

Kama utaota ndoto inakupa MATUMAINI katika safari ya maisha haswa ya kiroho n ahata ya kimwili; ujue kabisa bila shaka ndani yake kwamba ni MUNGU amesema nawe.

Sasa kwasababu NDOTO ni malango ya ulimwengu wa roho; kupitia ndoto hizo za kiroho mambo unayoota yanakuja kuwa dhahiri; yanatokea. Ulimwengu wa kiroho una athiri sasna ulimwengu wa kimwili.

Lazima utatambua kuwa hii ndoto ni MBAYA na INATISHA… hivyo basi ni shetani ndiye anasema nawe… Maana yake umeacha malango wazi hata shetani akapenya kusema nawe.

Kwa maana hiyo; unaweza sana kutofautisha NDOTO ZA KIROHO kwamba ipi ni ndoto ya MUNGU ama ipi ni NDOTO ya shetani.

No comments:

Post a Comment