Sunday, April 17, 2022

Je, ni halili mkristo kuolewa ao kumuoa muislamu?

 


Jibu langu ni "Hapana", Lakini natumai utasoma vizuri maelezo yangu hapo chini ili kuelewa ni kwa nini nimesema "hapana".

»Itakuwa vyema tukitumia biblià kufahamu mkristo ni nani na muislamu ni nani.

»MKRISTO ni mtu aliyeokoka kwa kuamini  kufa na kufufuka kwa Kristo na anamfuata Bwana Yesu. Tunaliona hili katika kitabu cha WARUMI 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua katika wafu; utaokoka".

»Tunapomuita Yesu kuwa ni Bwana yaani Bwana Yesu, tunamaanisha kuwa yeye ni kiongozi au mtawala wa maisha yetu  tukifanya yote ayatakayo (MATHAYO 7:21).

»Kwa hiyo Mkristo hujibidisha kumpendeza Mungu, hata kama kuna muda ataonekana kushindwa(kuchelewa kuolewa), hapaswi kumkana Yesu. Kama ataziacha amri za Mungu, hatoweza kuingia katika ufalme wa Mungu pamoja na kwamba hapa duniani alijiita kuwa yeye ni Mkristo.

MUISLAMU NI NANI?
»Pamoja na maandiko mengi ya kiislamu kutakakufanana na ya Kikristo(kwa sababu walinakili), lakini imani ni tofauti na tofauti zake ni nyingi mno ukizichunguza kwa makini.

»Waislamu huamini Yesu kuwa ni nabii, hawaamini kuwa Yesu ni Mungu, wala hawaamini kuwa Yesu alifufuka. Hii ndio sababu ya Wakristo na Waislamu kutokuwa sambamba, kwa sababu wanaamini vitu tofauti kuhusu kiungo muhimu katika Ukristo yaani Yesu (WARUMI 10:9).

»Katika YOHANA 3:18 tunaona kuhusu Yesu " Amwaminiye yeye(Yesu) hahukumiwi(hana hatia); asiyemwamini(Yesu) amekwisha kuhukumiwa(ni mwenye hatia); kwa sababu hakuliamini jina pekee la mwana wa Mungu".

»Muislamu ni mwenye hatia, aliyehukumiwa tayari kwa sababu hamwamini Yesu.

»Tukisoma katika 2 WAKORINTHO 6:14-17 "Msifungiwe nira  pamoja na wasioamini........yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini?......." Mkristo hapaswi kuolewa na muislamu.

»Hata kama mwanamke(mkristo) amefiwa na mume yaani ni mjane, anaruhusiwa kuolewa na mtu yeyote amtakaye katika Bwana tu. 1 WAKORINTHO 7:39 " ....yu huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye; katika Bwana tu".

»Hii ni amri ya Mungu na ni hekima pia, kwa sababu Mungu anatuambia mahusiano ya ndoa ni moja ya mambo yanayotusaidia kukua(kuimarika) kiroho na kuwa na nguvu za Kimungu na hayapaswi kutuzuia kukua kirohi.

»Kwa hiyo basi, wanamume wameamriwa kuwapenda wake zao na kuwafanya kuwa watakatifu(WAEFESO 5:25-33). Je, mwanamume wa kiislamu anaweza kufanya hivi hali yeye mwenyewe hamwamini Yesu? Jibu ni hapana hawezi badala yake ni kukuangusha kiroho na kukufanya uigeukie miungu ya kigeni ambayo ni chukizo kwa Mungu wetu.

»Tafuta kuwa karibu na Mungu, usikate tamaa kwa kuona umri umeenda wala huolewi; mwombe Mungu naye atakupa kwa wakati wake tena aonao kuwa wafaa.

»Je, unamfuata Yesu au unamwita Bwana, Bwana hali huyatendi yale asemayo? Je, unahakika kuwa ukifa unaingia mbinguni?

No comments:

Post a Comment