Sunday, April 17, 2022

Jifunze kuusu Pasaka

 »Neno "Pasaka" linatokana na neno la kiebrania "PESACH"  kwa kiingereza ni lenye maana "PASS OVER" yaani "KUPITA JUU YA".


»Mwanzo wa Pasaka ulikuwa ni wakati wa nabii Musa (KUTOKA 12:14,17-18,21, KUTOKA 13:3-4; HESABU 9:21-30).

»Pasaka ni tendo la Bwana kupita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, pale alipoiona damu ya mwanakondoo wa Pasaka katika vizingiti vya juu na miimo miwili ya milango yao alipita juu na kuacha kuwaharibu. Walioharibiwa walikuwa ni Wamisri ambao alama ya damu haikuonekana katika nyumba zao (KUTOKA 12:21-30).

»Mungu aliwaagiza wana wa Israeli kuikumbuka siku hii.

»Siku kuu hii ya Pasaka ilifanyika kuwa kumbukumbu kila mwaka katika mwezi wa Kiyahudi unaoitwa " NISAN" (NEHEMIA 2:1) au  "ABIB" (KUTOKA 13:3-4). Siku kuu hii ilifanyikwa kwa juma moja yaani siku ya 14 hadi siku ya 21.(KUTOKA 12:14,17-18; HESABU 9:1-5).

»Mwezi wa "NISAN" au "ABIB" katika kalenda yetu ni kati ya mwezi "MARCHI" na "APRILI". Kuanza kwa mwezi ABIB kunategemeanana mwandamo wa mwezi . Ndiyo maana tarehe za siku kuu ya Pasaka hubadilika kila mwaka, Lakini huwa ni kati ya mwezi Marchi na Aprili.

»Katika kusherekea siku kuu hii walihitajika kuchinja wanyama wengi sana ili kupata damu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kama ondoleo la dhambi. Kwa wastani katika kipindi cha Pasaka walichinjwa wanyama 256,500 (laki mbili hamsini na sita elfu na mia tano).

»Katika kusherehekea Pasaka, Wayahudi walifanya mkutano mkubwa  au konferensi ambapo walikusanyika pamoja na kula na kunywa na kuwa na muda mrefu wa kulisikia Neno la Mungu.

»Siku kuu hii iliendelea hadi katika kipindi cha Yesu Kristo. Yesu kristo mwenyewe alikuwa akienda kusherekea Pasaka(LUKA 2:41-52; YOHANA 2:13,23).

»Hiki kilikuwa ni kivuli cha Yesu Kristo kama mwanakondoo wa Pasaka aliyechinjwa msalabani.

»Yesu kristo alitolewa kusulubishwa wakati wa pasaka kama Pasaka wetu(YOHANA 18:39, 19:14-18; 1 WAKORINTHO 5:7). Kwa sababu hiyo, sasa hatuna haja ya kuchinja wanyamatena kama sadaka bali ni kumwamini Yesu ambaye ndiye sadaka yetu.

»Kila amwaminiye Yesu Kristo kwa Imani tu, damu ya Yesu hunyunyizwa juu yake na kuoshwa dhambi zote na kuwa salama(1 PETRO 1:2). Sasa hakuna haja tena ya kuchinja wanyama.Sasa tunaingia patakatifu pa Bwana(hekaluni) kwa damu ya Yesu(WAEBRANIA 10:19). Shetani ni Mharibu lakini hawezi kumharibu yeyote aliyenyunyiziwa damu ya Mwanakondoo (1 PETRO 1:2; UFUNUO 12:11).

»Kila asiyemwamini Yesu ghadhabu ya Mungu inamkalia, amekwisha hukumiwa (YOHANA 3:3,16-18). Kwa jinsi hiyo basi, ni busara mtu kusherehekea Pasaka pale tu ambapo amekwisha nyunyiziwa damu ya Yesu na kumshinda Shetani. Kinyume cha hapo, ni kufanya mchezo wa kuigiza(YOHANA 1:35-36, 10:10).

Imeandaliwa naye MS. Guillain
Mount Moriah Ministry of God
#Kenya 
Kwa huduma zaidi, wasiliana nasi kwenye nambari +254714981516 ao kwenye baruwa pepe mountmoriahministry@gmail.com

No comments:

Post a Comment