Thursday, April 14, 2022

Upendo unafaa kwa mkristo ao kwa kila mtu?

Ujambo mpendwa, ninakuja kukwambiya kwamba mda unaisha jaribu angalao kuwa na upendo kwa wale wanao kuudhi, kudharau, kuchukiya maana maandiko inasema wapendeni wanao wauzi. 

Kristo ni UPENDO,na yeye ndiye sababu ya sisi kusamehewa dhambi, maana isinge likuwa upendo wa Mungu kwetu sisi, Nani angelisimama? 

Upendo, Ni Sheria ao Amri tulio pewa na Mungu, tupendane Kama ndugu. Upendo usitiri dhambi, unapo mpenda jirani yako hauta musengenya, musema vibaya ao kutowa ma lalamishi mbaya sababu utakuwa unampenda. 

YESU KRISTO amekubali kufa kwa ajili yako na Mimi SABABU alitupenda. 
Tafuteni amani na watu wote, na muifwatiliye. Inanahana Mungu anaitaji kwetu kudumisha amani Kati Yetu. 

Upendo unafaa kwetu sisi kama wanadamu maana KRISTO amekufa sio kwa ajili ya dini bali kwa ajili ya Ulimwengu.

Kwa swali ao pendekezo yeyote, tutimiye batuwa pepe kwenye mountmoriahministry@gmail.com ao weka comment yako hapo chini, Asante 🙏🙏🙏

Wednesday, April 6, 2022

Kwa neno lako

Luc5:1-6 

[1]Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,

[2]akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao.

[3]Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.

[4]Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.

[5]Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.

[6]Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;


Petro alikuwa bora sana katika urowaji lakini ujuzi haikumufanya apate samaki siku iyo. Inamaanisha kwamba kuna kitu ao utalaamu fulani petro aliitaji sana ili kupata samaki wengi. Nayo ilikuwa kukutana na Yesu Kristo. 


Mtumbwi imekataa maji, sababu ilijuwa leo nisiku kubwa sipashwi kuvuwa ao kukaribisha mtu mwengine tofauti na Kristo. Kabla ya shuguli inabidi kwanza ni mpokeye yeye aliye Mkuu kuliko chochote. Ndiposa maandiko inasema kwamba 


⬇️⬇️⬇️⬇️

Mimi Bwana ndiye nitakae kutanguliya mbele yako. 

KUMBUKUMBU LA TORATI 31:8 

Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha, usiogope wala usifadhaike. 


Ndio mana baada ya mission being accomplished petro amerowa samaki wengi. Petro alikuwa under stress, machozi, usingisi maana alikuwa napenda kulala sana na nafikiri siku iyo petro akufika nhumbani sababu alikuwa ajapata kitu. 


Kilicho mfanya petro stress imuishe ni kukubali kuachiliya chombo chake kiweze kuifikisha injili siku iyo. Amekubali wito na baada ya kukubali Jesus amejitukuza kwake.

⬇️⬇️⬇️⬇️

Mahali akili yako inaishiya ndiko ya Mungu inaanziya, usiogope maana Mungu yu pamoja nawe kila siku na kila wakati, haijalishi hali unayo ipitiya.

Kama uleshindwa kabizi Mungu shida, vikwazo na vyote avichukuwe yeye. 

Yesu alikuwa na shabaa na petro sio mtumbwi, petro hakuwa na lolote lakufanya maana alikuwa tayari ameisha give up mapema.  Na vile gisi mpango wa Mungu uko kila siku perfect God akunyamanza, alimwambiya petro baada tu ya kumaliza ebu egesha mtumbwi wako kule, pale.

Petro akasema KWA NENO LAKO NITAFANYA

Sunday, April 3, 2022

Maisha ya ukristu wa leo

Ujambo mpendwa, natamani ku share nawewe jambo hili, ni kwa nini wakristu waleo wanapenda ao kutamani sana baraka lakini hawapendi kuhubiriwa kuusu dhambi? Unadhani shida nigani? Asante kwa mchango wako. uwe na wakati mwema. 🙏🙏🙏  

Vifungo vya laana

Neno LAANA katika kamusi limetafsiriwa kama ukosefu wa radhi za mwenyezi Mungu, hasira ya Mungu. Au ni apizo atoalo mtu kwa mtu mwingine ili afikwe na ubaya, uovu, msiba au hasira ya Mungu. LAANI  limetafsiliwa kama, shtakia kwa Mungu, au ombea uovu.


Zipo laana nyingi lakini leo ningependa kuzungumzia laana zifuatazo:-


Ukoo/familia:- laana zinazojiendeleza kwenye ukoo hutokana na matokeo ama matunda ya dhambi. Kwa mfano unakuta katika familia husika kuna wengine wana laana za magonjwa sugu kama kansa, kwenye hiyo hiyo familia wengine hawaolewi, wengine wameolewa lakini ndoa hazidumu, wengine hawapati mimba. Familia nyingine utakuta kuna vifo vya ghafla, wanaanza maisha na kufanikiwa na kuwa na mali na biashara kubwa au kazi lakini mwisho wao wanaishia kufilisika na kufa kwa mateso makali.Unatakiwa kuomba maombi ya rehema na toba na lazima utamke kilichofanyika na matokeo yake.  Kwa sababu kila dhambi iliyofanyika ni kutokana na kuwa na miungu mingine. Dhambi inatokea pale mtu anapomwacha Mungu wa kweli na kusikiliza miungu mingine. Sasa unapokosa msaada wa Mungu wa kweli unapata misaada ya miungu inayokusababisha wewe kutenda kinyume na Mungu. “Usiwe na miungu mingine ila Mimi- Kumbukumbu la torati 5:7”

Laana za kulaaniwa na mtu mwingine:- Yawezekana ulikosana na rafiki yako ama mtu mwingine pengine mwalimu wako wa shule akakuchukia na kukulaani. Anaweza kukulaani kuwa na kamwe hutakaa uendelee kwa kila utakalofanya usifanikiwe.

Laana za kujilaani mwenyewe:- Kuna watu hawaridhiki na jinsi walivyo ama niseme viungo vya miili yao, yaani kwa ufupi hawajikubali ama kujiamini. Utakuta mtu analalamika na kusema “aah mimi kwa ufupi huu sidhani kama nitakaa nipate mwanamke mrefu atakaenipenda, ama mwingine atajilaani kwa kusema kamwe hawezi kuwa mtu wa kwanza darasani kwa sababu tu ya mtu fulani nyumbani kwao hajawahi kuwa” Siku zote maneno huumba na kujiumba, kwa maana hiyo yale uyatamkayo mdomoni kwako vivyo hivyo yanafanyika.

Laana ya vitu visivyoisha: Kuna watu wamelaaniwa kwa kila wakigusacho kisiendelee na matokeo yake hujikuta wameanzisha vitu mbali mbali bila hata kimojawapo kukamilika. Mfano mtu anataka kujenga lakini anaishia nusu na kuanza kitu kingine ambacho nacho hakifiki mbali. Nataka kuanzisha biashara ya nguo, atanunua sehemu ya kuuzia nguo lakini hakuna kitakachoendelea. Watu kama hawa ni wale wanaonena kwa midomo lakini hawatekelezi.

 Laana ya kufanya tendo la ndoa na dada yako au kaka yako, baba yako au mama yako

Kuna mambo mengine sio rahisi hata kuelezea lakini yapo na yanafanyika mtu amelala na Dada yake, mwingine na kaka yake, laana ya Mungu imeagizwa juu yao “Kumb 27:22 Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye au Binti ya mamae. Na watu wote waseme Amina”


Haya yote yanatokana na UPOFU wa mawazo. Akili ikifungwa mtu hawezi kufanya maamuzi yoyote. Pia akili ikifungwa mtu haoni ugumu wa dhambi. “2Wakorintho 3:14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi wakati lisomwapo Agano la kale, utaji uo huo wakaa, yaani haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo”. Soma pia Waefeso 4:18

NAVUNJAJE VIFUNGO?

Biblia inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii ina maana ya kuwa kuna watu wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Watu hawa wamefungwa kwenye magereza na Ibilisi.

Tutambue ya kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha kwamba kuna mahali ambako tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye mwenywe kuingia kati yetu.

Aliyahidhirisha haya kwenye kitabu cha nabii Isaya 61:1-2 Roho ya Bwana Mungu i juu yangu kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”.

Vunja uhusiano wako na hiyo miungu pamoja na kazi zake na agano lililofanyika kati ya familia au ukoo wako na hiyo miungu. Kila unapotamka mwisho wake sema kwa sababu nimesamehewa. Ipo mistari mingi ya kuvunja maagano lakini mimi nitakupa kifungu hiki cha mstari katika kuvunja maagano na mapoozo ya aina yoyote. “Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya kutiwa mafuta” Isaya 10:27

Kifungu kingine ambacho waweza tumia ni kwa kutaja maneno haya wakati wa kuvunja vifungo ama laana “Bwana Yesu, nasimama mbele zako na katika ulimwengu wa roho, kujiachanisha nafsi yangu (Taja jina lako) na vifungo vya kuzimu kwa upande wa baba yangu na mama yangu kwa sababu nimesamehewa.” Endelea vivyo hivyo kwa kutaja, roho na mwili kwa kutumia maneno hayo hayo uponyaji hufanyika katika nafsi, mwili na roho.

Mtegemee Roho Mtakatifu kwa maana atakufundisha mengi ikiwemo kuomba na maagizo ya Yesu. Na kwa kufuata maagizo ya Yesu na kuenenda kwa roho hivyo vifungo vya nafsi vitakwisha. Soma Wagalatia 5:16-25, Luka 22:40-46. Kudumu katika maombi, kuenenda kiroho na kuepuka uovu ni muhimu kwa sababu kwa kufuata misingi hiyo ndipo unafunguliwa vifungo kwa kuombewa ama kwa nguvu inayotenda kazi ndani yako kupitioa roho mtakatifu. Lakini pia ni muhimu kujua ya kwamba sala ya toba pekee haitoshi kumfungua mtu kama ana vifungo na sio imani tu bali na juhudi binafsi ya mtu itasaidia katika kumuweka huru. Wapo watu wanaotaka kupokea miujiza bila ya kuwa na mabadiliko yoyote, ama bila kusoma neno la Mungu na kukua kiroho ama bila kuomba. Wao husubiria siku za maombi, ama mikesha ama makongamano ya maombi ili waombewe kisha baada ya hapo hawajishughulishi katika kukua kiimani.

Kuwa hodari katika Bwana ili upate ulinzi wa Mungu. Waefeso 6:10-11 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani”

Maana ya kuwa hodari katika Bwana ni kukaa kwenye maombi, kusoma na kulishika neno lake liwe ndani yako, na kutaka kumjua yeye zaidi. Sikuzote Sali kwa bidii katika kupambana na muovu shetani ndo mana tunaambiwa vaeni silaha zote za Mungu ili kuweza kupingana na hila za muovu shetani.


Mbarikiwe na Mungu!

MS. Guillain 

Mount Moriah Ministry of God, Mwinjilisti/Muandishi


Saturday, April 2, 2022

Jinsi ya kutambuwa manabii wa kweli

Katika somo hili  nitaelezea jinsi ya kuwatambua manabii wa kweli wa Mungu kutokana na sifa walizokuwa nazo wakati wa Agano la Kale na  Agano Jipya. Ni muhimu kila mkristo aliyeokoka  aweze kupambanua (kutofautisha) na kutambua manabii wa kweli na manabii wa uongo. Manabii wa kweli  walikuwa na sifa zifuatazo;  1.Walikuwa waaminifu. Hapa tutaangalia manabii watatu ambao ni Yesu, Musa na Samweli ambao walikuwa waaminifu katika mambo yote ya Mungu. Waebrania 3:1-2 “...Yesu aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama naye Musa alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.”  Katika andiko hili, Yesu  amefananishwa na nabii Musa alivyokuwa mwaminifu.  Mwingine ni Samweli, alipokuwa mzee aliwashuhudia wana wa Israel jinsi alivyokuwa mwaminifu tangu akiwa kijana. 1Samweli 12:2-4 “Basi sasa, angalieni, mfalme anakwenda mbele yenu; na mimi ni mzee, mwenye mvi; tena, tazameni, wana wangu wapo pamoja nanyi; nami nimekwenda mbele yenu toka ujana wangu hata leo. Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za BWANA, na mbele ya masihi wake, nalitwaa ng’ombe wa nani? Au nalitwaa punda wa nani? Au ni nani niliyemdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi. Nao wakasema, hukutudhulumu, wala hukutuonea, wala hukupokea kitu kwa mkono wa mtu awaye yote.”  2.Walikuwa wakisema kile ambacho Mungu aliwaambia au kuwaonyesha bila kuongeza au kupunguza. 2Petro 1: 21 “Maana unabii haukutolewa popote  kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu”.  3.Walikuwa na bidii kuutafuta  uso wa Mungu. Hapa nitawataja baadhi ya manabii ambao walikuwa wanaomba mbele za Mungu kwa bidii ambao ni; Yesu Kristo Bwana wetu, Eliya Mtishibi na Ana. Soma katika Biblia: Luka 22:41, Luka 2:36-37 na Yakobo 5:17-18.  4.Walikuwa wanyenyekevu na wenye hofu ya Mungu.  5.Walikuwa na huruma kwa ajili ya Taifa lao na kuliombea ili Mungu asilihukumu kutokana na makosa ambayo lilifanya. Hapa nitawataja baadhi yao ambao ni Musa na Samweli. Samweli 12:23 “Walakini mimi, hasha!  Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka.”   Kutoka 32:31-32 “Musa akarejea kwa BWANA akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu. Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.”  6.Waliyoyatabiri yalitimia. Lakini kwa nyakati hizi za mwisho ni muhimu kwa kila mwamini kuwa makini na kufahamu ya kwamba siyo kila nabii asemaye unabii ukatimia na kutenda  miujiza ni nabii wa kweli. Kumbukumbu 13:1-3 “Kukizuka katika yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia, akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikilize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto…”  Kutokana na andiko hili hapa juu linaonyesha wazi ya kwamba tunaweza kuwatambua manabii wanaopotosha kwa mambo yale wanayotuambia au kutuelekeza kinyume na neno la Mungu. Na  ikiwa hawana matunda mazuri hao ni manabii wa uongo. Ndio maana imeandikwa;  Mathayo 7:15-20 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa - mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! watu huchukua zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.” Mfano wa  mti mwema ni yule mtu anayeyafanya mapenzi ya Mungu (matakwa ya Mungu). Na mfano wa mti mwovu ni mtu  asiyeyafanya mapenzi ya Mungu.  7.Unabii walioutoa ulilingana na neno la Mungu. Haukupigana na neno la Mungu mahali popote katika biblia. Mwamini anaweza kuutambua unabii kwa kutumia neno la Mungu. Lakini ni lazima kwanza ayafahamu maneno ya Mungu na kuyahifadhi moyoni. Wakolosai 3:16 "Na neno la Kristo na likae kwa wingi  ndani yenu katika hekima yote…” Mtu akiwa na maneno ya Mungu kwa wingi moyoni anaweza kuyapima mambo yote ya Kiroho.  Jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo. Ni kwa njia  zifuatazo; 1. Tunaweza kuwatambua au kuwapambanua kwa tabia zao  ambazo haziendani na neno la Mungu na ziko dhahiri wala haziwezi kufichika. Tunaweza kuwatambua kwa kutumia  neno la Mungu na tunda la Roho.   Wagalatia 5:22-23 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”  2. Kuwatambua kwa mafundisho yao ya kibinadamu. Mafundisho yao wameyatunga hayaendani na neno la Mungu. Wanafundisha na kuhubiri kwa kutafsiri mistari ya biblia kinyume neno la Mungu. Kwa sababu hiyo wanakuwa wamewapotosha waamini katika njia ya Mungu. Hutumia  mafundisho ya uzushi na uongo na kuyachanganya na maandiko ya neno la Mungu kana kwamba ni neno la Mungu. Kwa sababu hiyo huwapotosha wasiolijua neno la Mungu kwa ukamilifu. Ikiwa mwamini yuko makini na anayafahamu maandiko  kwa ukamilifu ni lazima atagundua ya kwamba mafundisho wanayofundisha na kuyahubiri yanapingana na neno la Mungu katika biblia. Ndio maana imeandikwa tusiamini kila roho (kila nafsi) tuzijaribu kwanza. 1Yohana 4:1 “Wapenzi msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.”  Mwalimu wa neno la Mungu. Ni muhimu kuwa makini anapotafsiri mistari ya neno la Mungu katika biblia, ni lazima ahakikishe inaendana na maandiko mengine katika biblia. asichokijua kwa usahihi  asiwafundishe watu na kuwapotosha ili asije akahukumiwa. Imeandikwa;  Ufunuo wa Yohana 22:18-19 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”  Kumbukumbu 4:2 “...neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu, niwaamuruzo.” Katika maandiko haya, Mungu ameonya tusije tukaongezea katika maneno yake ambayo yamekwisha kuandikwa. Kwa sababu hiyo hatupaswi kuchanganya neno la Mungu na mafundisho yetu ya kibinadamu. Pia ameonya  tusiondoe wala kupunguza maneno  ambayo yamekwisha kuandikwa kwenye kitabu chake.  Jambo lingine limpasalo mtu kutambua ni kwamba maandiko yaliyomo katika biblia ni maneno ya unabii. Ufunuo wa Yohana 22:19 “Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.” Maneno ya unabii ni yale ambayo Mungu alisema na manabii wake kwa njia ya sauti, maono na ndoto, yakaandikwa katika biblia. Kwa sababu hiyo mtu anapofundisha neno la Mungu anakuwa anafundisha maneno ya unabii. Kwa kufanya hivyo si kwamba ametoa unabii.  Unabii Unavyotokea Nabii anatoa unabii kwa yale ambayo Mungu amesema naye kwa njia ya sauti, maono na ndoto. Hesabu 12:6-8 “Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo;  Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?”  Tahadhari Kuhusu Kutoa Unabii. Ni muhimu kila mkristo aliyeokoka kuwa makini ili asije akahukumiwa kwa mambo haya yafuatayo; 1.Usitabiri uongo 2. Usipokee unabii wa uongo. Yeremia 14:14,16 “Ndipo BWANA akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya mioyo yao. Na watu hao, waliopewa unabii na wao, watatupwa nje katika njia kuu za Yerusalemu kwa sababu ya upanga na njaa; wala hawatakuwa na mtu wa kuwazika, wao na wake zao, na wana wao, na binti zao; maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.”  Yeremia 23:31-32 “Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema, Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA.”  3. Kuwa makini usiseme mambo ambayo Mungu hakusema na wewe kwa njia ya sauti, maoni na ndoto. Utakayoyasema hakikisha au thibitisha ni Mungu kweli amesema. Mungu anataka useme neno lake kwa uaminifu. Yeremia 23:28,31-32 “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA. Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema, Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi(...)